
MARCESH FOUNDATION : RESTORE A CHILD PROJECT
RESTORE A CHILD
Restore a child ni project Iiyoandaliwa na taasisi! ya MARCESH FOUNDATION ambayo imejikita Katika masuala ya Elimu.Project hii malengo mbalimbali kwa vijana wadogo hususani walioko Katika shule za sekondari,shule za msingi na vituo vya kulelea watoto waishio katika mazingira magumu.Lengo kuu ni kuwajenga vijana na kuwaminisha wanaweza kufika mbali Katika safari zao za mafanikio kuanzia umri mdogo.
SHUGHULI ZINAZOFANYWA KATIKA PROJECT HII
1=Kugawa mahitaji ya shule kwa wanafunzi walioko hatarini kuacha shule kutokana na changamoto za ukosefu wa vifaa.
2= Kutoa Elimu ya jinsia na kujutambua kwa vijana.
3.Kutoa elimu dhidi ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi yao.
4.kufundisha namna na njia mbalimbali za kufikia kuanzia umri mdogo na kukabiliana na changamoto zinazowakumba.
5.Kurejesha tabasamu kwa jamii kwa kusaidia mahitaji mbalimbali na kurudisha matumaini kwa waliokata Tamaa.
MALENGO YA PROJECT HII
1.kuhakikisha wanafunzi wanaotokea familia duni hawaaachi shule kutokana na changamoto za kimaisha
2.Kuhakikisha kijana anajitambua tangu umri mdogo.
3.Kuhakikisha ukatili wa kijinsia unatokomea kuanzia Katika ngazi ya familia.
4.Kuhakikisha vijana wadogo wanakuwa na mafanikio na mfano bora kwa jamii.
5.Kuhakikisha vijana wanapata elimu kuhusu namna mbalimbali za kukabiliana na changamoto wanazokutana Nazo.
6.Kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora hii ni pamoja na kuboresha miondombinu ya kujifunzia.
KAULI MBIU
Nimechaguwa kuwa mzazi
Unaweza Kushiriki kwa changia vifaa vya shule
Kwa taarifa zaidi tafadhari wasiliana nasi kwa simu namba +255 711 700 229
SNL ADMIN
Leave a comment
Your email address will not be published. Required fields are marked *